admin's Guestbook
|
Loginto leave a new post in the guestbook.
admin
says:
Je Ndoto zipi zenye maana?
Ndoto zenye Ujumbe ni zile tu ambazo unaziota kati ya 9 usiku mpaka saa 1 asubuhi wakati huo mwili unakuwa umepumzika na umeshamaliza kazi ya kusaga chakula. Je Ndoto zipi ambazo hazina maana? Ndoto ambazo hazina ujumbe ni zile ambazo. unaziota mapema usiku au mara tu unapolala. Ndoto unazoota wakati ukiwa na matatizo ya Tumbo au ukiwa mgonjwa. Ukiwa umelala sehemu yenye kelele nyingi nje kama ngoma au disko au umelala katika chumba chenye joto jingi au ukiwa wewe mwenyewe umelala vibaya. Ndoto ambazo unaota ikiwa chumbani kwako kuna televisheni au radio inawaka. Tafsiri ya ndoto kwa ujumla: Ukiota katika ndoto kitu chochote chenye Ncha kali kama kisu, mkasi, panga, shoka, msumari sindano na jamii ya vitu hivyo ndoto hiyo inaashiria wewe uliyeota kupata habari mbaya za kifo, au kufungwa, ugonjwa,kufukuzwa kazi, kuibiwa, kutapeliwa, moto Ukiota katika ndoto kitu chochote chenye kungara au cheupe, iwe nyumba gari, nguo, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kupata "bahati nzuri au mambo mazuri." Kupata pesa, kupata mchumba,safari yenye faida, kupata cheo, kupona mgonjwa,kuzaliwa mtoto Ukiota katika ndoto kitu chochote kichafu au kisichopendeza, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kupata upinzani na bahati mbaya. Kama kupingwa katika mambo yako, kufanyiwa fitna kazini au katika biashara, kutorokwa na mke au mpenzi, kupoteza mali, kuibiwa,kupigwa, kukamatwa au polisi kupata ajali Ukiota katika ndoto unapanda Juu kwa njia yoyote ile kama vile kupaa, kupanda ngazi kupanda kwa kamba, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kupata mafanikio ya kimaisha, kadri unavyozidi kupanda ndio mafanikio yatakuwa zaidi Ukiota katika ndoto unashuka au unaanguka kwa njia yoyote ile, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kukwama na kupata pingamizi katika mambo yako, kadri unavyozidi kwenda chini ndio kiwango cha kuharibikiwa kwa mambo yako Ndoto za kuota unastarehe zina maana tofauti ziko za bahati mbaya na zipo za bahati nzuri, kwa mfano ukiota unafurahia labda ngoma au harusi au tafrija au unacheza mziki uliokufurahisha, hiyo kwa muotaji itakuwa dalili ya mafanikio.
lakini kama ukiota uko katika sehemu hizo na hufurahi yale yanayoendelea hapo hiyo ni dalili ya kupata bahati mbaya. ukiota umekuwa tajiri basi utapata umasikini Ukiota umepoteza maana yake utapata |
